KSHG Münster
Home |  Kontakt |  Newsletter |  Impressum 
Junge Kirche

 
 AKTUELLES:

Karibuni katika mtandao (website) wetu wa KSHG Münster!

Jumuiya wazi
Matukio – Vyakula – Maisha ya furaha
Utamaduni – Elimu – Ubunifu
Ibada – Imani – Maisha ya Kiroho
Msaada – Ushauri – Maisha ya Undugu

Hiyo ndiyo ”parokia katoliki ya wanafunzi” (KSHG) ya mji wa Münster / mkoa wa Westfalia.

Karibuni
Baraza la parokia la KSHG, mwezi wa kumi, mwaka 2005

Sisi ni kanisa, taifa la Mungu, katika chuo kikuu (university) na vyuo mbali mbali (universities of applied sciences) vya Münster. Sisi ni wanafunzi, tunaojitambua kuwa jumuiya ya kikristo, kwa ajili ya wanafunzi wenzetu wa vyuo vyote vya mji wetu hapa Münster. Hivyo tunawakaribisha sana ninyi nyote ili mtufahamu kwa njia hii ya mtandao wetu.

Mungu na Dunia

Tunasherekea imani yetu – kwa namna na ibada mbalimbali. Kwa pamoja tunafurahia kuimba na kusali, kumsifu Mungu na kumwabudu. Yote hayo tunayafanya katika Misa zetu za Jumapili hapa kanisa la Mtakatifu Petro; pia katika sala na ibada mbalimbali ndani ya kanisa letu dogo, na katika vikundi mbalimbali vya kubadilishana maoni na mawazo.

Karibuni

Misa za kufungua muhula katika kanisa kuu la Münster:

Misa za kufungua na kufunga muhula katika Kanisa Kuu la Münster ni moja ya matukio muhimu sana katika shughuli zetu. Misa hizi za kufungua na kufunga muhula ni kivutio kikubwa cha vijana wanafunzi hapa Münster. Mara kwa mara wanafunzi wapatao elfu moja, wa kila kitivo na kila idara ya chuo kikuu, hujumuika nasi katika ibada za misa za kufungua na kufunga muhula. – Kwa hakika hili ni jambo la pekee sana hapa nchini kwetu Ujerumani.

Sanaa na Ubingwa

Sisi ni Jumuiya yenye vipaji – tunatoa ushuhuda wa furaha yetu kiimani katika muziki, nyimbo, michezo na kwa njia nyingine za kisanii. Mara kwa mara, hapa mgahawani petu „Milagro“, hufanyika maonyesho ya wasanii vijana chipukizi. Kadhalika katika shule ya mchezo ya kuigiza („Placebo“), wanafunzi hupewa nafasi ya kuvivumbua na kuviendeleze vipaji vyao vya maigizo jukwaani. Na katika Kwaya na Okestra yetu, mtu anaweza kushamiri katika muziki (akitumia ala au sauti tu). „Vumbua vipaji vyako!“ – Hii ndio kaulimbiu yetu hapa KSHG.

Karibuni

Karibuni

Jumuiya yetu huandaa na kuratibu majadiliano jukwaani na Prof. Dr. Norbert Walter, Mtaalamu mahiri wa Uchumi katika masuala ya mabenki hapa Ujerumani.

Kwa namna hii, tunazidi kujielimisha kwa njia ya majadiliano, mikutano, na vikundi vya masomo. Pia tunaangalia maswala ya kisiasa, ya kiuchumi, ya kiekolojia (kimazingira), ya kijamii na ya sayansi mbalimbali. Tunajitahidi kuwezesha mazungumzo kati ya walimu na wanafunzi katika vitivo tofauti hapa katika chuo kikuu chetu. Hii ni nafasi muhimu ya kutoa ushirikiano ambao mara nyingi wanafunzi tunaukosa tuwapo mashuleni.

Ushauri na Huduma

Karibuni

Jumuiya yetu imejizatiti kuwahudumia wanafunzi wageni ambao wanatafuta malazi hapa Münster. Hasa wale ambao wamefika hapa Münster mara ya kwanza kutoka ng’ambo. Hawa tunawasaidia kufahamiana na watu mbalimbali. Pia endapo wanahitaji ushauri na msaada hasa katika masuala ya uongozi wa kiroho, au msaada wa kimasomo, tunajitaidi kuwasaidia. Jumuiya yetu hutoa ushauri, hasa ushauri wa kibinafsi ama msaada wa dharura kwa wale wanaohitaji. – Sisi tupo kwa ajili yenu!

Kwa wale amabo wanaiishi nchi za nje na pia wale ambao wanasoma Münster tuna- wakaribisheni sana na tuko tayari kuwahudumia. Endapo unapenda kuwasiliana nasi, au endapo una swali, au maoni, basi tuma barua pepe kwenye anwani ifuatayo: kshg@bistum-muenster.de

Tunawakaribisha sana Münster katika jumuya yetu! Asanteni!

Na kwa sasa: Enjoy surfing!




Zurück zurück zum Seitenanfang zum Seitenanfang Artikel versenden Artikel versenden
Artikel drucken Artikel drucken
Aktuelles
Café Milagro
der aktuelle Speiseplan im Milagro ...mehr
Aktuelles
Aktuelles
letzte Änderung: